Mama wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia
Kampuni yake ya Fabak Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale
litakalofanyika Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri
kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya
Tanzania hasa katika nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30
kutoka sehemu mbali mbali ambao nao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.
Watu Maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo
kuonyesha Mavazi ya Khanga za Kale kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous
Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutokana na onyesho hilo imepangwa
kupelekwa kwenye Kituo cha Kulea watu walioathirika na Madawa ya Kulevwa
kilichopo Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani.
Comments