MSONDO KUKABIDHIWA VYOMBO VIPYA NA KAMPUNI YA KONYAGI

Katika habari nzuri kwa muziki wa dansi wiki hii ni sherehe ya Msondo Ngoma kukabidhiwa vyombo vipya na kampuni ya Konyagi siku ya Ijumaa pale Leaders Club. Kupatikana kwa vyombo hivyo kutaleta burudani zaidi na changamoto kubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Msondo, ambayo ni moja ya bendi za zamani kuliko zote nchini Tanzania imejiwekea heshima ya kuwa ikienda na wakati na hivyo kuweza kuwa na wapenzi nchi nzima na hata nchi jirani, katika uhai wote wa bendi hii.





Comments