Kwa muda barabara ya Magomeni kwenda Sinza kupitia Tandale eneo la
Somanga, Magomeni makuti, ililazimika kufungwa kwa magari ili kupisha
umati mkubwa wa watu waliokuwa wakisindikiza mwili wa Mariam Khamis
kwenda katika mahala pake pa mwisho duniani. Mariam ambaye alikuwa
muimbaji wa bendi ya TOT Taarab alijulikana sana kwa wimbo wake 'Paka
Mapepe' alipoteza uhai wake jana katika hospitali ya Muhimbili, kutokana
na matatizo baada ya kujifungua. Ukubwa wa umati ule ni kielelezo
kikubwa kuwa marehemu alipendwa na watu. Mungu ailaze Roho yake pema
peponi Amin
Comments