HUSSEIN MKIETY aka SHAROMILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

Msanii wa vichekesho aliyekuja na staili mpya kabisa katika ulimwengu wa comedy Tanzania, na ambaye pia aliingia katika fani ya muziki wa kizazi kipya na kupata mafanikio mazuri,Hussein Mkiety maarufu kwa jina la Sharo Milionea amefariki dunia jioni hii, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Sharobaro, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza ambapo pia ndio nyumbani kwao.Wiki hii imekuwa ya misiba katika tasnia ya sanaa kwani wiki hii msanii wa maigizo Mlopelo amezikwa, na bado msanii mwingine John Maganga anategemewa kuzikwa kesho Jumanne katika makaburi ya Kinondoni.
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMIN

Comments