EPIC BONGO STAR SEARCH TOP 5 WAINGIA FAINALI


Walter Chilambo (EBSS12)

Nsami Nkwabi (EBSS06)
Nshoma Ng’hangasamala (EBSS07)

Salma Abushiri (EBSS09)

Wababa Mtuka (EBSS11)
Baada ya mchakato wa miezi kadhaa hatimae Epiq Bongo Star Search(EBSS) inafikia tamati. Mchujo uliokuwa na mambo mengi yenye furaha na uchungu hatimae wanamuziki watatno wamebakia ili kuchukua ushindi wenye zawadi ya fedha, mkataba wa kurekodi nyimbo toka Zantel, sifa, na jukwaa la kuweza kujiendeleza katika ulimwengu wa muziki, jukwaa ambalo mwanamuziki yoyote yule angependa sana kupewa.
Washiriki waliotinga katika  fainali hizo ni Nshoma Ng’hangasamala (EBSS07), Walter Chilambo (EBSS12), Wababa Mtuka (EBSS11), Nsami Nkwabi (EBSS06) na Salma Abushiri (EBSS09).

Kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na wasanii mbalimbali wa hapa nchini kama vile Rich Mavoko, Omi Dimpoz, Ben Paul, Lina, Amini, Mzee Yusuf, Haji Ramadhan, Mwasiti, Ditto, Laila Rashid, Linex na Barnaba, katika shughuli itakayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 9 November 2012.

Tiketi za shindano hilo zimeanza kuuzwa katika maeneo tofauti kwa sh 70,000,  sh 30,000 pamoja na sh 10,000 viti vya kawaida.

Comments