Skip to main content
WASANII WA ARUSHA WALAANI KUDHARAULIWA
TATIZO LA WASANII KUDHARAULIWA NA MAAFISA UTAMADUNI NI LA KAWAIDA SANA HAPA NCHINI SIKU HIZI, WENGI BADO TUNAKUMBUKA AFISA UTAMADUNI MUSOMA ALIPOAMRISHA WASANII KUWEKWA NDANI KWA SABABU AMBAZO MPAKA LEO HAZIJAJULIKANA. JUZI AFISA UTAMADUNI MMOJA HAPA DAR ALIKUWA AKIJITAHIDI KUZUIA TAMASHA LA UTAMADUNI LISIFANYIKE, SASA SIJUI YEYE KAZI YAKE INA MAANA GANI KAMA HAKUNA MAONYESHO YA UTAMADUNI. KWA SISI WASANII WENGINE AMBAO TULIWAHI KUISHI KATIKA SERIKALI AMBAPO MAAFISA UTAMADUNI WALIKUWA CHINI YA WIZARA YA UTAMADUNI, NA KILA AFISA ALIJITAHIDI WASANII WAKE WAWE BORA ZAIDI, KWA KUWA MAAFISA UTAMADUNI WALIKUWA WOTE WAKIFUATA MWONGOZO MMOJA WA WIZARA YA UTAMADUNI MATATIZO KAMA HAYA YALIKUWA MACHACHE, KIUKWELI ILIKUWA MARA NYINGINE NI KERO KWANI KAMA KULIKUWA NA SHUGHULI YA NYUMBANI WASANII WA NYUMBANI WALINYIMWA HATA KIBALI CHA KUTOKA NJE YA MKOA KWANI WAO WALIKUWA NDIO WENYEJI WA SHUGHULI. INASIKITISHA SANA KWANI ARUSHA HIYO NDIO ILIKUWA KATI YA KURUGENZI YA KWANZA HATA KUWA NA BENDI YA ILIYOMILIKIWA NA KURUGENZI YA ARUSHA. ARUSHA KILIKUWA NDIO KITUO KIKUBWA CHA WANAMUZIKI NA BENDI MAARUFU NYINGI ZILIANZIA AU KUHAMIA ARUSHA.......
Wasanii wa
muziki wa kizazi kipya na vikundi mbalimbali vya maigizo mkoani Arusha
wamewataka viongozi wa serikali kutowadharau na kuwashirikisha
kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo jijini hapa
Hali hiyo
imetokea wakati zikiwa zimebaki siku chache ili kufanyika uzinduzi rasmi
wa Jiji la Arusha baada ya wasanii hao kudai kutoshirikisha kwa lolote .
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake msanii wa muziki wa kizazi
kipya Nakaaya Sumari alisema kuwa wameshangaa sana kusikia kuwa msanii
kutoka dar es salaam Diamond Platnum atakuja kutumbuiza ilihali wao
wapo na hawana taarifa yeyote.
Nakaaya
alisema kuwa hawana tatizo na Nasibu Abdul (Diamond) ambaye amealikwa
kuja kusherehesha uzinduzi huo ila walichokiona ni dharau kutoka kwa
afisa Utamaduni wa manispaa kwa kutoonyesha ushirikiano na badala yake
wamepewa taarifa ya kufanya kitu juuya uzinduzi huo kama zima moto jana
usiku baada ya wao kuulizia.
“Tumeshanga sana hii ni dharau wasanii wa arusha hatuheshimiki kabisa na
tumeuliza ndo tunaambiwa eti tuandae kitu kwa ajili ya uzinduzi dah
yani inakatisha tamaa sana alafu afisa utamaduni mwenyewe anatuona
anatupotezea”alisema nakaaya
Hata
hivyo Nakaaya alimpongeza Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwa
kutoa ushirikiano wake kwao na kuahidi kushirikiana nao kwa madai ya
kilichofanyika ni makosa ya kibinadamu.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa arusha Hussein Sechonge
alikemea vikali tabia hiyo kwa kuwa wasanii wana mchango mkubwa wa
kufikisha ujumbe na kuwataka viongozi kuwa wazalendo.
Aidha
walimtaka afisa utamadumi manispaa Juma Sule kutoa ushirikiano kwa
wasanii wa hapa kwa kuwa wao ndio wanajua kila kitu kuhusu manispaa na
sio Diamond.
”tunamshangaa sana hapa kuna wasanii 70 sasa nashangaa kwenye mwenge
aliletwa Juma Nature wakati wao wapo hapa na hawafahaamu kitu chochote
sio vizuri”alisema Sechonge.
Hadi jamii
blog inaondoka katika ofisi za manispaa wasanii hao walikuwa nje ya
ofisi ya meya wakisubiri kujadiliana namna ya kufanya na kumaliza
tofauti hiyo. HABARI NA PICHA TOKA http://pamelamollel.wordpress.com/
Comments