LEO nimegundua maficho ya hii bendi mpya. Nimewakuta hapo wakiwa bizy wakifanya mazoezi kwa ajili ya onyesho lao la kila wiki pale Thai Village Masaki. Kundi zima hili hapaa
Immaa kwenye Bass Gitaa |
Allan Kiso, alipitia awamu ya kwanza ya Mapacha Watatu |
Amose, nilisha wahi kumuona Kalunde huyu enzi hizo |
Daud kwenye Tumba |
Baraka |
Athumani kwenye keyboards...hata B Band aliwahi kupitia |
Mkongwe Joniko Flower, anajulikana tokea enzi za Chuchu na alipitia Machozi |
Sam Machozi ndie huyu |
Sonny Masamba si sura ngeni kwa waliowahi kuwa wapenzi wa Diamond Sound |
Vyombo vinarekibishwa na Juma |
Kushaba- Vocalist na meneja, kwa wale wafuatiliaji wa Tusker Project Fame sura hii si ngeni |
Mary Lucas alipitia Borabora Sound na wapenzi wa BSS lazima wanamkumbuka huyu |
Comments