Jumamosi tarehe 13 Oktoba
katika ukumbi wa Welfare Center, mambo makubwa mawili yalifanyika, kwanza vijana wengi walioshiriki na wale
waliokuja kufuatia Kabati Katiba Star Search walipata elimu nzuri ya Katiba ya
Tanzania. Na pili ilikuwa burudani kwa kwenda mbele kutoka kwa vijana
walioshiriki Star Search kuonyesha vipaji vyao. Vijana 150 waliweza kujitokeza
kuonekana mbele ya jopo la majaji
majaji Eddo Bashir (Ebony Fm), Temmy Mahondo (Country
Fm), Dj Ammy Yeyo (Country Fm ), Agnes Anderson (Ebony Fm) na Dj Muba wa (Ebony
Fm) . Mchujo uiofanyika baada ya hapo uliwezesha vijana 20 kuingia katika
Top Twenty ya mpambano huo. Tarehe 27 Oktoba ndipo itakapoingia awamu ya pili
ya shindano hili na Top Ten kupatikana.
Comments