Katika kuhamasiisha vijana wa
Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika
kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM
Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua KABATI KATIBA STAR SEARCH. Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya
Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha,
na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili
kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA
STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo
mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya
kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne
na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba
vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii
inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa
wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.
Comments