MUIGIZAJI WA NOLLYWOOD AFUNGWA MIEZI 3 KWA VITENDO VYA USHOGAMsanii mwuigizaji wa filamu toka Nollywood, Bestwood Chukwuemeka  mwenye umri wa miaka 28 wiki hii amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu bila faini kwa kushiriki vitendo vya kishoga.
Akijitetea mahakamani alikubali kuwa alimtendea jamaa aiyekuwa amelala nae baada ya wote wawili kulewa kupita kiasi, na hivyo kuomba mahakama impunguzie adhabu.Vitendo vya kishoga ni kosa la jinai chini ya kifungu 284 cha Penal Code ya Nigeria. Hakimu alionya kuwa adhabu ile ingekuwa funzo kwa vijana wengine ambao hujificha kwa mwamvuli wa ulevi ili kuvunja sheria. Siku alipokamatwa alijitetea kuwa alidhani alikuwa na mpenzi wake waliekuwa wakinywa nae club muda mfupi kabla ya hapo. Sheria ya Nigeria inayokataza mapenzi ya jinsia moja imeweka kifungo cha miaka 14 kwa wakosaji.

Comments