Ratiba za bendi wakati wa Idd


Idd ndio hiyo inakuja, mambo yatakuwa mataaamu, hizi ni baadhi ya ratiba za bendi zetu siku ya Idd Mosi na Idd pili;

-MAPACHA WATATU(wajuba wawili) Idd Mosi- Nyama Chabe Tegeta na Iddi Pili watakuwa White House pale Kimara Korogwe na baada ya siku hizo mambo yatakuwa kama kawa Jumanne Coco Star Club na Ijumaaa Mikocheni Resort Centre

-XTRA BONGO-Idd Mosi White House  Kimara, (mchana na usiku/) Idd Pili-Meeda Bar  SINZA

-MASHUJAA-Idd Mosi wako Masasi ukumbi wa  Emirate, Idd Pili watakuwa Mtwara, ukumbi wa Makonde

- FM ACADEMIA-Idd Mosi- New Msasani Club Kuanzia saa 9 mchana

- MSONDO NA SIKINDE-Idd Mosi Leaders Club. IDD Pili Zanzibar pale Gymkhana Club

-KALUNDE BAND –Idd Mosi  watakuwa TRINTY Oysterbay

-MARK BAND-Wako Cairo, Misri Idd Mosi na Idd Pili

-KILIMANJARO BAND- Idd Mosi Salender Bridge Club

Huko Nzega katika ukumbi wa New Ephra Hotel, Idd Mosi na Idd Pili kutakuweko African Beat Band chini ya Mafumu Bilali Bombenga, nae Bi Khadija Kopa atakuwepo huko tarehe  1, Septemba 2012 kutoa mipasho yake ya nguvu


Comments