Ras Makunja baada ya kupokea Tuzo |
Bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani Ulaya, Ngoma Africa Band siku ya Jumamosi 11,Agosti
2012, walishambulia jukwaa na la International Africa Festival 2012,Tubingen, Ujerumani,
na kuhakikishia washabiki kuwa FFU burudani kali ya muziki. Bendi hii ambayo imejizolea sifa kubwa kutokana na uwezo wake wa kulishambulia jukwaa, ilionyesha umahiri wake na hatimae kiongozi wa bendi hii, alipokea tuzo ya kimataifa ya
"International Diaspora
Award" kwa niaba ya bendi hiyo.
Comments