Mkutano wa viongozi wa bendi uliokuwa umeitishwa na BASATA na CHAMUDATA, umekwama kufanyika. mkutano huo ulitangazwa kwanza kuwa utafanyika Afri Center lakini hatimae ukatangazwa kuwa utafanyika katika ukumbi wa BASATA shariff Shamba kuanzia saa tano, hadi ilipofika saa saba na nusu hakukuweko na maelezo yoyote kwanini hakukuwa na mkutano, mkutano umekwama licha ya kuhudhuriwa na baadhi ya wawakilishi wa bendi. Baadhi ya waliokuweko ni Nyoshi Sadat wa FM Academia, Meneja wa bendi ya Akudo, na John Kitime wa Kilimanjaro Band. Hakuna sababu iliyotolewa zaidi ya kuambiwa mkutano utaitishwa tena
Comments