Mwanamuziki Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama Koffi Olomide, ambaye karibuni katoka kwenye mashtaka ya
kubaka huko Ufaransa, amepewa kifungo cha nje cha miezi mitatu kwa kumjeruhi
producer wake baada ya ugomvi uliotokea kati ya hao wawili kwenye hoteli moja
mjini Kinshasa.
Mwezi
Februari katika jiji la Paris Ufaransa, wacheza show wake watatu walimfungulia
mashtaka ya kuwabaka na kuwafungia ndani kinyume cha sheria, Kofi alikana haya
mashtaka na kurudi zake Kinshasa.
Hili
jipya limetokea baada ya Kofi kukutana uso kwa uso na Producer huyo Diego
Lubaki anaejulikana zaidi kama Diego Music, na Kofi kuanza kumdai producer huyo
fedha ambazo alimlipa watengeneza video lakini kazi hiyo haikufanyika.
Ngumi zikaanza
kurushwa na mabaunsa kadhaa walilazimika kuamua tifu hilo, na Kofi akawekwa
chini ya ulinzi. Ingawaje Lubaki baadae alitaka kufuta mashtaka, Hakimu aliamua
kuendelea na kesi. Kofi akapatikana na hatia ya kumjeruhi Lubasi lakini
mashtaka yaliyoambatana ya kuharibu mali ya hoteli(mlango mmoja ulivunjwa)
yalifutwa na hakimu. Kofi alifika mahakamani na wanasheria kumi.
Katika kesi yake ya
kubaka wanasheria wa Kofi walisema masteji show waliitunga ili wapate vibali
vya kuishi Ufaransa.
Comments