Shilole akana hana mtoto mgonjwa

Msanii Zuwena Mohammed maarufu kwa jina la Shilole, ameongea na blog hii na kulalamika kuwa kuna mtu anatumia jina lake na hata amefungua ukurasa wa Facebook akitumia picha zake na kufanya utapeli kwa kutumia jina lake. Jipya linaloendelea wakati huu ni blog kadhaa kuweka taarifa kuwa Shilole anaomba msaada maana ana mtoto anaumwa ambaye anatakiwa kwenda India. Shilole amekataa katakata kuwa na tatizo kama hilo. Kwa ujumbe huu tunawataarifu chungeni sana maana kuna uwezekano wa watu kutapeliwa

Comments