Ngoma Africa band kupewa Tuzo la kimataifa, " IDA - International Diaspora Award"

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" au maarufu kwa jina la "FFU"wazee wa virungu na makombora ya muziki, yenye makao yake nchini Ujerumani, imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza muziki wa Afrika kwa kasi duniani,na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu la " IDA - International Diaspora Award"  award hiyo inatolewa na taasisi za kimataifa, itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja wa FFU siku ya Jumapili ya 12-8-2012 katika sherehe maalum za Gala night zitakazo hudhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo watu maarufu duniani.
Sherehe za kukabidhiwa tuzo hiyo zitafanyika mjini Tubingen, mkoa wa Baden württemberg, kusini mwa ujerumani.
Taasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanzia mwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya kiafrika inayolitangaza bara la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu wa kuzipigia kura bendi
hizo katika tovuti mbali mbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia ushindi wa mamilioni ya kura, pia imegundulia kuwa bendi hiyi inakubalika na mamilioni  ya washabiki wa mataifa mbali mbali, 
Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni 50 duniani kote, hali hii inatishia maporomota wa muziki wa kimataifa, kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya washabiki,ni bendi ambayo kipenzi
cha mamilioni ya washabiki......www.ngomaafrica.com

Comments

Anonymous said…
Kamanda ras makunja na kikosi chake nawapa hongera sana,kamanda anajituma
jukwaani kwake kuna vituka vya kila aina,ulinzi wake wakati mwingine ni utata mtupu
Anonymous said…
wafuasi milioni 50 wa ffu ni pamoja na bint wa gadaf? au yule alikua mshikaji wa karibu wa boss