Utamaduni katika maonyesho ya Karibu Travel and Tourism Fair 2012


Karibu Travel and Tourism Fair ni onyesho la kimataifa la shughuli mbalimbali zinazohusiana na Utalii. Maonyesho haya yamekuwa yakifanyika katika viwanja vya Magereza kwa muda wa siku tatu kila mwaka.Kama ilivyo kawaida sana hapa Tanzania maswala ya utamaduni hayapewi nafasi ambayo yanastahili kwa hiyo kukosesha mapato makubwa katika mtandao mzima wa Utalii Tanzania.





Taarifa inayofuata inatoka kwa mtu aliyehudhuria maonyesho haya yalioisha hivi karibuni......... Masuala ya utamaduni na burudani katika Tamasha hili kwa kiasi fulani yamekuwa katika kiwango duni sana sijui ni kwa mtazamo wangu ama vipi, lakini hayo ni maoni yangu. Zaidi ya kuona baadhi ya vikundi vya ngoma asilia visivyozidi 3 vilivyo pooza, nilikutana na kundi hili la muziki wa 'live' linalojulikana kama Aqua Band, linaundwa  na wanamuziki mchanganyiko  ambao kati yao kuna mwanadada mmoja.Wana set ya vyombo vizuri sana na vyenye nguvu, tatizo ni production sii nzuri kabisa kama vile niliona kama hawakujiandaa kufanya onyesho katika mkusanyiko wa kuuza utalii wa Tanzania. Wanapiga muziki wa copy wakati wote, ambao lazima nikubali walicopy vizuri na wenye muelekeo wa uasilia wa watunzi wake. Nadhani watatyarishaji wa Maonyesho haya wanatakiwa kutoa umuhimu zaidi kwa kuelewa kuwa Utamaduni pia ni jukwaa zuri sana katika biashara ya Utalii.....

Comments

Anonymous said…
ha ha ha ha ha, mr john... kweli ndo kazi yako hii?