Kundi la Taarab la Dodoma Stars Music Club limo katika
mazoezi makali ya kujifua ilikurudisha heshima ya kundi hili kongwe. Niliwakuta
wanamuziki wa kundi hili wakiwa katika mazoezi makali kutokana na waimbaji wengi kuwa wapya na bado ni
wachanga katika fani hii. Kundi hili limekuwa chimbuko la wanamuziki wengi wa
Taarab akiwemo Ally Star, ambaye alipata jina la Star kutokana na kuweza kuokua
jahazi kwa kupiga kinanda na kuimba peke yake akisaidiwa na mke wa mzee Jela, baada ya wanamuziki wote wa kundi hili
kuhama ghafla wakati kikundi kililazimika kupiga katika harusi fulani
Comments