Baadhi ya wanamuziki wa awamu mojawapo ya Atomic Jazz |
Nimepata waraka huu kutoka kwa mwanamuziki mkongwe Benno Villa Anthony...................................Mkuu, kwanza kabisa namwomba Mwenyezi Mungu akujalie roho ya
uvumilivu ktk kufuatilia taarifa hii. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu,
nilikuwa na kipindi cha mahojiano na Manju wa muziki na mtangazaji wa TBC,
komredi Masuud Masuud. Kwa vile kipindi kilirudiwarudiwa na huku Manju akitamka
namba yangu ya simu, wengi waliinukuu, na kati ya hao walioinyaka ni Mzee John
Mbulla, aliyekuwa mpiga sax wa Atomic Jazz. Mzee huyu kwa sasa kweli anaumwa
sana. Zaidi ni maradhi ya macho, haoni. Kumbe kwao ni Mpwapwa ila kwa sasa
anahifadhiwa na diwani wa Kibaigwa, Ndugu Richard Kapinye.......0717
303070. Baada ya kusikia kuwa wasanii wanachangiana ili kupata tiba,
Diwani huyo alinipigia na nikazungumza nao wote wawili. Wameniomba nikupe
taarifa hii ili uitoe kwenye vyombo vya habari, ikiwezekana apate msaada wa
tiba. Diwani anasema kuwa John akipata operation ya macho atapona na kuanza
kujitegemea maana nguvu bado anazo. KUMBUKA...Mzee John Mbulla ndiye aliyepiga
Saxaphone kwenye wimbo wa "TANZANIA YETU NDIYO NCHI YA KUSIFIWA",
wakati Mbaraka Mweshehe alipojiunga na Atomic Jazz kwa
muda..............Mkuu Kitime, Nina uhakika kama wana Media wakimtembelea na
kutoa habari zake, naamini wengi wataguswa na kumsaidia. Natanguliza
shukrani zangu za awali. Asante Mkuu.
Comments
wanamuziki mkongwe,Dar.