Ratiba ya Mazishi ya rafiki yetu Steven Kanumba


Saa 2:30 asubuhi:  Mwili wa marehemu Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni.

Wito unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.

Saa 3:30 asubuhi:  Mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Saa 4:00 asubuhi: Misa ambayo itachukua dakika 60, ambapo itafuatiwa na salamu kutoka kwa watu mbalimbali.

Saa 6:00 mchana: Mwili wa marehemu kuanza kuagwa ratiba iatakayoendelea mpaka saa 9:00 alasiri, ambapo safari ya kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya Kinondoni itakapoanza, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.

Saa 10:00 alasiri: Mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.

Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua ili kumuaga kwa heshima.

Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.

         
K.N.Y GABRIEL MTITU                               MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI



Comments