African Stars "Twanga Pepeta" kuwa ziarani mikoa ya Ziwa. Mwanza, Musoma, na Shinyanga







The African Stars Band, Twanga Pepeta, inataraji kufanya ziara ya maonyesho katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Mara. Ziara hiyo inataraji kuanzia  Mwanza siku ya Ijumaa tarehe 30-03-2012.

Kesho yake siku ya Jumamosi tarehe 31-03-2012 kundi zima la Twanga Pepeta litakuwa katika ukumbi wa Musoma Club, pale Musoma na kumalizia ziara kwa kufanya onyesho la nguvu  mjini Kahama siku ya Tarehe 01-04-2012 katika ukumbi wa Club Dimpoz.
 Twanga Pepeta wanatumia ziara hii kwa ajili ya kutambulisha albamu yao inayotamba sasa hivi ya Dunia Daraja yenye nyimbo za 'Dunia Daraja', 'Mapenzi Hayana Kiapo', 'Kauli', 'Umenivika Umasikini', 'Mtoto wa Mwisho' na 'Penzi la Shemeji' pia watatambulisha baadhi ya wasanii waliojiunga hivi karibuni wakiongozwa na Prince Mwinjuma Muumini Kocha wa Dunia, Venance Geuza, Jumanne Said, Grayson Semsekwa na Mshindi wa Shindano la 'BSS Second Chance' Hajji Ramadhani ambae anakuja rasmi kwa ajili ya kuwapa shukrani wapenzi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kumpigia kura mpaka kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika shindano.

Comments