The Q Band
Jana nilipata text message kunikaribisha kwenye bendi pale VIP Lounge Maryland Bar Mwenge. Niliona ni muhimu kupita kupata vitu vipya. Nikakuta bendi yenye wanamuziki kadhaa wazuri ninaowafahamu. Nilimkuta mwimbaji mzuri sana Bi Leah Moudy ambaye alipata umaarufu baada ya kushiriki katika kile kipindi cha Bongo Star Search. Pia nilimkuta mpiga drums ambaye niliwahi kuwa naye Tancut Almasi Orchestra, Bwana Kejeli Mfaume, pia mpiga bass mahiri ambaye nae alipitia Tancut Almasi na nikaja kumkuta akiwa na TOT Band. Q Band wako Maryland kila Alhamisi.

Comments