Mashujaa Band waandaa Listening Party


Nikiwa na wanamuziki wenzangu Mafumu Bilali, Anania Ngoliga na Hamza kalala, tulikaribishwa na uongozi wa Mashujaa Band katika ukumbi wa nyumbani kule Vinginguti ili tukasikilize nyimbo mpya za Mashujaa Band. Katika kitu ambacho ni nadra katika bendi nyingi, bendi ilikuwa iko tayari kupata ushauri toka kwa wapenzi na waalikwa kuhusu nyimbo zao mbili mpya. Ushauri ulitoka mwingi toka kwa viongozi mbalimbali wa bendi na wapenzi waliokuwa wameruhusiwa kuingia na kusikiliza nyimbo hizo.
 Baada ya utambulisho wa  shughuli toka kwa Chalz Baba, Mashujaa Band ilileta show yao mpya ambayo imekuwa ikiratibiwa na msanii wa siku nyingi Dodoo.
Baada ya show nyimbo ya kwanza ambayo ni utunzi wa Chalz Baba iliyoenda kwa jina la Kidole Risasi ilipigwa. Maoni baada ya wimbo yalihusu urefu wa wimbo, ambao ulionekana kutokana na uwingi wa waimbaji katika bendi na wote kuwa na vipande vya kutuma katika wimbo, hivyo kuufanya wimbo uwe mrefu sana. Jingine lilikuwa ni kugundua kuwa wapiga magita walikuwa wakipiga bila ya kutyuni magitaa. Kulikuweko na mawazo kuhusu uchezaji wa show, ambapo wengi walikubaliana kuwa show ilikuwa safi katika onyesho hilo tofauti na kawaida katika madansi mengine. Pia ulitolewa ushauri kuwa mafundi mitambo walikuwa hawajiipatia kazi yao ya kurekibisha vyombo sawasawa. Mpiga tumba na wale mabingwa wa kurap waliambiwa waongeze ubunifu.


















Comments