Kilimusic Awards 2012 yazinduliwa


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo wamezindua  mchakato wa kuwatafuta na kuwapa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2011.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager bwana George Kavishe alisema Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:

1. ACADEMY:
ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya hamsini hadi mia moja, kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao watawekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekidhi vigezo vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Jan 2012.

2. MAJAJI:
Hatua ya pili ni Majaji, ambapo majaji watakuwa na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi.  Jopo hili hujumuisha wadau wa tasnia ya muziki kumi na tano (15).

3. KURA:
Hii ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa muziki watapiga kura zao kuchangua washindi ambapo kwa shindano la mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia sabini (70%) na kura za majaji asilimia thelathini (30%.). Katika kufanikisha upigaji kura kutakuwa njia zifuatazo za upigaji kura nazo ni:
. Njia ya ujumbe mfupi (sms).
. Njia ya barua pepe (Email).
. Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
. Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)

Comments