Kamati ya kusaka vazi la Taifa yazinduliwa

Mheshimiwa Waziri Dr. E Nchimbi akiwa na Naibu wake kwenye uzinduzi huo.
Mheshimiwa Waziri wa Utamaduni, Habari na Michezo Mheshimiwa Dr E Nchimbi, leo katika ofisi yake amezindua kamati ya vazi la Taifa. 
Kamati hiyo ina wajumbe wafuatao;
1. Joseph Kusaga- Mkurugenzi Clouds Media, Mwenyekiti wa Kamati
2. Habib Gunze -  Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA
3. Joyce Mhavile -  Mkurugenzi Mtendaji ITV na Radio One
4. Absalom Kibanda - Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari
5. Makwaiya wa Kuhenga -  Mtunzi wa vitabu, mwandishi na mwendeshaji wa kipindi cha Je, Tutafika?
6. Mustafa Hassanali- Mbunifu wa mavazi
7. Ndesamburo Merinyo - Mbunifu wa mavazi
8. Angela Ngowi - Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni, Katibu wa Kamati

Mwenyekiti wa Kamati Joseph Kusaga (kulia) akiwa na baadhi ya wanakamati
Kamati itategemewa kuendesha mchakato wa kuja na vazi la Taifa na kutoa ripoti tarehe 28 Februari 2012 kwa mheshimiwa Waziri.

Comments