Teddy Mbaraka mpiga Bezi wa Wahapahapa afiwa na baba yake

Teddy Mbaraka akiwa na cap nyekundu, kulia ni Paul Ndunguru

Kushoto mpiga bass Andy Swebe akiwa na mpiga bass mwenzie Teddy Mbaraka
Mwanamuziki mkongwe na mahiri Teddy Mbaraka amefiwa na baba yake huko Pemba. Teddy ambaye pamoja bendi nyingine amekwisha pigia bendi kama Chezimba, Tatunane, na sasa Wahapahapa. Amefiwa na mzazi wake jana Jumamosi 24 September. Mwanamuziki Tom Nhigula ambaye alifiwa na baba yake wiki chache zilizopita ndie alikuwa na jukumu la kusambaza taarifa hiyo kwa wanamuziki wengine. Katika kipindi cha wiki chache zilizopita wanamuziki kadhaa wamepoteza baba zao akiwemo pia Karola Kinasha. Mungu awalaze wazazi wetu hawa pema peponi. 
Amina.

Comments