Hatimae Cesilia Edward aenda India kwa matibabu.

Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu. Cecilia Edward ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopo New Delhi -India kwa matibabu,Jumatatu  tarehe 26, Septemba 2011.
E Mungu msaidie Cesilia aweze kupona. 
Amen!

Comments