Umeshapata bahati ya kukutana na wanamuziki hawa?
Kundi hili la wanamuziki, hutembea toka sehemu moja mpaka nyingine. Unaweza kuwakuta mtaani au kwenye sehemu za starehe kama baa. Nadhani wanahitaji meneja mzuri na ni wasanii ambao katika nchi nyingine wangekuwa tayari wamekwisha fanya ziara nyingi za nje ya nchi. Na kwa vyovyote wangekuwa na album sokoni, lakini nchi hii waliokamata mpini wa biashara ya muziki ni kizungumkuti.

Comments