Cool James mtoto wa Dandu

Cool James, Mtoto wa Dandu au CJ Massive zilikuwa aka za James Dandu. Mwanamuziki aliyezaliwa 1970  katika jiji la Mwanza.
Alianza shughuli za muziki mwaka 1983, lakini album yake ya kwanza aliitoa 1986. Akajiunga na mwanamuziki kutoka Kenya Andrew Muturi na kuanzisha kundi la Swahili Nation. Na wakaweza kutoa single iliyoitwa  Mapenzi. Mwaka 1990 alijitoa kundi hilo na kuanzisha kampuni yake Dandu Planet Mwaka 1993 akiwa na Black Teacher alitoa album iliyokuwa na vibao kama Dr Feelgood, iliyoweza kushinda tuzo la Best Scandinavian Dance Track 1994, pia kulikuwa na nyimbo kama Godfather na The rhythm of the track. Alianzisha kampuni nyingine Dandu Entertainment na kufanya kazi kadhaa kupitia wanamuziki wa Afrika Mashariki. Dandu hatasahaulika kwa wale wanaofahamu chanzo cha tuzo za kila mwaka za muziki za Kilimanjaro Music Awards ambazo zilianza kwa jina la Tanzania Music Awards (TAMA). Alifariki katika ajali ya gari tarehe 27 Agosti 2002 akiwa na umri mdogo wa miaka 32.
Mungu amlaze pema peponi.


Comments