Nchini kwetu kuna waimbaji wengi. Waimbaji wengine ni maarufu sana lakini kiwango cha uimbaji wao kiko chini. Kuna waimbaji ambao wanajua kuimba na wanapewa sifa hizo na kuna wengine wana bahati mbaya licha ya kuwa waimbaji wazuri, huwa hawapati bahati ya kujulikana. Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa, Jose Mara na Kalala Junior ni waimbaji wa ukweli. Wana uwezo wa hali ya juu na wanautumia uwezo huo. Pia hawa ni wafanyakazi haswa wako jukwaani toka mwanzo hadi mwisho wakishirikiana kwa ile staili ambayo kwa wale waliokuweko katika miaka ya 70 ilitumiwa na Trio Madjesi, waimbaji watatu walioanzisha kundi la Orchestra Sosoliso
Comments