Kundi la Kalunde limekuwa sana kuanzia pale lilipokuwa na wanamuziki wachache chini ya Deo Mwanambilimbi miaka kadhaa iliyopita. Lazima sifa zitolewe maana makundi mengi yameanza tena kwa kishindo na kuishia hewani lakini hili limekuwa linakuwa kila mwaka. Kuingia kwa Bob Rudala na Anania Ngoliga kutaendeleza sana uwezo mkubwa wa kundi hili.
Comments