Super Melody ya DodomaKibonge

Super Melody ni bendi ya zamani hapa Dodoma nimeikuta ikiwa katika eneo moja Singida Road karibu na 4 way Bar, hapo  ndipo huwa wanpiga kila Jumamosi. Kati ya nyimbo ambazo ziliniletea kumbukumbu ya enzi ni walipopiga Tambola na Mokili wa John Bokelo, na Dada Lemmy wa Tabora Jazz. Ni burudani haswa

Comments

Anonymous said…
Bw.John Kitime,
Asante sanan kwa juhudi zako za kuzungukia sehemu na vilabu mbali mbali ili kutukusanyia habari za bendi na vikundi mbali mbali,Ombi langu na ninadhani ni jambo muhimu ni kuwa unapopita katika kumbi hizo na kupiga picha tu bila maelezo maalum na pia majina ya hawa wasanii,unatuacha katika giza,jitahidi kuwa unaandika na majina ya hawa wasanii chini ya kila picha unayopiga,hii itatusaidia sana kuwajua wasanii hawa kwa sura na majina pia.Natanguliza shukrani.
Mdau,Atlanta.GA,Usa.