Msondo Ngoma ziarani Moshi

Mnyalukolo Ridhwani Pangamawe

Said Mabela


Shaabani wa Dede
Juma katundu


Mama Nzawisa

Band kongwe ya muziki wa dansi hapa nchi , Msondo Ngoma Music band imewasili mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mualiko wa kiwanda cha kuzalisha sukari TPC, ili kushiriki katika siku ya familia ( Family Day) huko huko kiwandani TPC.
 Katika siku yao ya kwanza , hapo jana band hii ikiongozwa na Mkongwe Said Mabela ilifanya onesho lake katika ukumbi wa Aventure Africa uliopo mjini Moshi ambapo wapenzi wa muziki wa dansi, walijumuika kupata burudani.
Onesho hilo ambalo sehemu kubwa ya wapenzi walikuwa vijana wa zamani ama kama wanavyojulikana hapa Moshi kama senior citizens lilifana sana, haswa pale bendi hii ilipopiga nyimbo zake za zamani, zama za NUTA na JUWATA, nyimbo  kama vile Mpenzi Zarina, Nimeamua niwe mbali nawe, Fatuma na nyingine nyingi. Pia wakazi hawa walipata fursa ya kusikiliza nyimbo mpya kabisa ambazo bado hazijaanza kusikika redioni, na show kali toka kwa mnenguaji pekee wa kike ktk band hiyo maarufu kama Mama Nzawisa. Leo tarehe 18/6/2011 kundi zima la Wana Msondo Ngoma Music Band litakuwa katika viwanja vya Limpopo kiwandani TPC kuanzia mchana likitoa burudani kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho cha kuzalisha sukari.
 Burudani zaidi ilikuwa pale muimbaji mkongwe wa bendi hiyo Shaaban Dede aliposhindwa kumaliza kuimba wimbo wake maarufu kama Fatuma! baada ya kupandwa na hisia kali, bila shaka akikumbuka mbali na nafasi yake kuzibwa na Mzee Mabela. Ο€ata picha Mabera akiimba na kupiga solo.

Comments