Tchimanga Assossa na Bana Maquis

   Bana Maquis chini ya Tchimanga Assossa ni bendi nyingine ya kuzuru kama ni mpenzi wa zilipendwa. Bendi hii yenye wanamuziki wachache(chini ya kumi). Hupiga kila Ijumaa pale Jolly Club-Upanga. Nilipata raha pamoja na kusikiliza nyimbo nyingi za Assossa kama Huba, Ngalula, pia nilipigiwa live wimbo ambao Assossa alishiriki akiwa na Negro Succes wakati huo chini ya Bavon Marie Marie, kibao Maseke Ya Meme.


Ben, rafiki yangu huyu kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa Rainbow Connection, bendi ambayo ilikuwa chini ya nduguye aliyekuwa anaitwa Prince, mwanzoni mwa miaka ya 80. Wakati huo Prince aliekuwa 'seaman' alikuwa karudi nyumbani na kuanzisha bendi iliyokuwa na masikani yake New Africa Hotel. Patrick Balisidya pia alikuwemo katika kundi hili, japo nilipotaka kuomba kazi Patrick alinikataza na kuniambia si kundi la kukaa muda mrefu. Na kweli bendi ilikufa baada ya muda mfupi. Ben alikuwa kati ya wanamuziki wa waanzilishi wa Tancut, alihamia Tancut akiwa na Shaaban Yohana Wanted, wakitokea Morogoro katika bendi ya Les Cuban



Comments