VIJANA WA TANZANIA HUENDA WAPI KUPUMZISHA AKILI BAADA YA SAA ZA KAZI?

AWALI HAPA PALIKUWA NA JENGO LILILOITWA  NYUMBA YA SANAA WASANII WENGI WALIKUWA WAKIFANYA KAZI ZAO HAPA, KWA SASA KILICHOBAKI JINA WASANII HAWATAKIWI HAPA
NILISAMBAZA UJUMBE HUU ASUBUHI TAREHE 23JUNE 2017, BAADA YA MASAA KADHAA  WATU MBALIMBALI WAMECHANGIA .........

Je vijana wa Tanzania huenda wapi kupumzisha akili zao baada ya kazi? Hili swali bahati mbaya sana halimo katika ajenda ya viongozi wa Tanzania, hata wale viongozi wa makundi ya vijana. Hakuna anaewaza kubuni miradi ya kutengeneza sehemu za aina hiyo, hata viwanja au majengo ambayo viongozi wa zamani waliyaweka kwa shughuli hizo 'social centers', viongozi wa sasa wanazivunja na kuporomosha majengo ambayo wao huita miradi na kusahau kabisa kuwa vijana wanastahili kuwa na maeneo ya kupumzisha akili. Ziko wapi social halls zilioachwa na akina Joseph Nyerere? Ziko wapi community centers zilizoachwa na wakoloni? Matokeo ya dhambi hii ni vijana kuishia kukutana katika kumbi za bar na vijiwe visivyo rasmi. Hahihitaji akili nyingi kujua kuwa mazoea ya kufika katika maeneo ya aina hiyo huzalisha mapenzi ya ulevi wa pombe na hatimae dawa za kulevya. Na hakika kukosekana kwa burudani mbadala huishia vijana kuona burudani nyingine pekee ni ngono. Sikiliza tungo za nyimbo na hadithi za vijana wa leo, angalia video na filamu asilimia kubwa  ni kutukuza pombe na ngono. Uvaaji na uchezaji wa mabinti ni wa kuelekeza kuwaza ngono, si ajabu kukuta moja ya biashara zinazolipa ni guest houses. Utumiaji mkubwa wa dawa za kulevya ni matokeo ya kukosekana sehemu halali za vijana kukutana kupeana mawazo bora. Tulikomboe Taifa la kesho kwa kuhakikisha si kuhamasisha viwanja vya michezo tu, pia maeneo ya shughuli nyingine za kijamii za vijana. Si kila kijana anapenda au anajua kucheza mpira, hivyo kuhamasisha kutenga  viwanja vya michezo tu hakika haitoshi.
John Kitime

FEEDBACK
1. Shukran kwa neno zuri
2. Vizuri sana mzee Kitime, kilichosababisha yote hayo ni umiminisaition, mdudu ambaye anaendelea kututafuna hadi sasa
3. Community Centers,zilijengwa na Mkoloni. Baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967. Kufuatia Sensa kubwa ya kuhesabu Watu. Ikagundulika kuwa. Watanzania tumeongezeka sana.  Hivyo mahitaji ya Tiba yakaongezeka kuliko Uwezo wetu wa kujenga hospitali. Ndipo ikaamuriwa Community Center ya Magomeni igeuzwe Hospitali. Ikafuatia ya Temeke. Ikajengwa Amana Hosp. Jirani ya Ukumbi wa Kijamii wa Amana. Weneyeji maeneo ya Mnazi mmoja ambayo ndiyo kata ya Mchafukoge kama  sikosei walikutana Anatouglou Hall. Jirani ya ilipo Amtubhai Hosp na Mnazi mmoja Hosp. Wenyeji wa Mitaa ya Jangwani walikutana Banda la Madobi ilpoimba pia Bendi ya Kilwa Jazz. Msimbazi/Morogoro Road. Ulikuwepo Ukumbi wa Tanzania Legions Uliotumiwa na Mashujaa wa Vita kuu ya Kwanza na ya pili. Umeuzwa juzijuzi na Watoto aidha Wajukuu wao!
4. Nimeona nchi kama ivory coast, Congo rd,zina kumbi  maalum Nzuri za muziki live kama vile Zenith uliopo Paris Ufaransa na sio ktk bar kama ilivyohapa kwetu,kuna mamia  wasioenda ktk muziki ama kujihusisha nao sababu ya mazingira yaliyopo hv  sasa
5. Kweli kabisa mkuu.Huku kwetu Kenya uko vivyo hivyo.Vijana hawashughulikiwi.Mambo yamebaki tuu ulevi,ngono,madawa ya kulevya na uhalifu.Its very sad indeed.
6. mijini  kulitengwa  maeneo ya wazi kwaajili ya michezo ambayo sasa    yamechukulkwa na wenye fedha kwaajili  ya faida binafsi,  mikoani kila wilaya ilikuwa na ukumbi wa utamaduni ambao sasa kumbi  hizo hakuna,  mkuu  kitime  umeona mbali sana
7. Kumbi nyingine zimekuwa totoro had sasa wameona bora wageuze nyumba za ibada, mfn ddc pale morogoro
8. Kilikua Kiwanja Changu Sana, tukishihudia vikundi kama Muungano, Mandela nk. Nikiwashuhidia watu kama Kuntu wa Kuntu, alikua Densa Mbilikimo, Chimbende km sijakosea,
Chidumule na Dr Remmy (R.I.P) na HAMISA wao.
Nk
9. Upo ukumbi wa juwata nao, umepoa kbs

10. Tanga Makorora Community Centre Ipo. Kama ni Gari, inatembelea RIM.
Kisosora Upo pia, nao halikadhalika. Nadhani Kumbi Hizi zingetumika kama ule wa AMANA kungekua walau na faida kwa vijana
11. Mawazo mazuri, binafsi naona ni kutokana na wataalamu wetu wabaosimamia sheria sijui ni kujisahau au ni vipi, maana hata miji mipya inayoanzishwa haiwi na mipango hiyo,, nikisema Wataalam wetu namaanisha kwamba Sera na mipango inaeleza vizuri juu ya kubakisha sehemu za social intertiment lakini haziwezi hata sehemu zao za Leaders club pia wameziua
12. zamani walikua wakijenga hizi community center na social halls kwa Halmashauri nyingi lkn kwa sasa hamna na zikizopo hazina hadhi tena kulingana na wakati
13. yaan kwa sasa kimtazamo wangu, km wizara husika, ikiwemo baraza, km ktk bajeti yake hakuna hii mipango, ina maana muziki wetu wa dansi, utahitaji taasisi nyingine kuuinua, kwani kutokuwa na public social Hall, kuna changia muziki wetu kuendelea kudorola. Nakumbuka sera za zamani kila kampuni au kiwanda au taasisi ilikuwa na sehemu ya burudani hata michezo, ndio maana had Leo miziki ya zaman itaendelea kukumbukwa sana kuliko hii ya sasa, haijalishi umehit mara ngap, utapigwa Radio mara kadhaa basi wanauchoka, inakuwa km "bublish " watafuna ikiisha utamu tu waitema.
14. mikoani na wilayani kunakua na hizo nyingi halafu miji mikubwa kunakuwa na viwanja vikubwa vya burudani vya kisasa vinavyomilikiwa na serikali
15. [09:31, 6/23/2017] ‪ Lkn hivi ktk bunge, cjasikia wabunge wakijadili hata uwepo wa hizi bendi zetu kongwe, mara nyingi wanaishia " kuselebuka " ,ebu wekeni "jojina " yaan wanacheza na kuimba tu
[09:33, 6/23/2017] ‪ Wana mchango mkubwa wa kuzirudisha hizi bendi zetu na kuzihuisha tena, zikawa na uhai na ushindani na bendi nyingine, kuliko kutegemea "Gate collections "
[09:35, 6/23/2017] ‪ Tukizungumzia hizi kumbi, lazima tuzizungumzie bendi zetu  pia, maana watakuja kusema, kumbi za nini wakati muziki wenyewe hauone kani dah, uwa naumia sn na huu muziki wetu.
16. nadhani tukipata mtu akawa ama Wazir ama mbunge itasaidia,vinginevyo vyama vya muziki haswa wa dansi,kama yatakubaliwa basi itakuwa poa,mfano sera ya mheshimiwa Rais ya Tanzania ya viwanda,wizara nayo ingetumbukiza mkono ikasema viwanda na burudani kuweka uanzishwaji wa viwanda kwenda sambamba na shughuli za burudani mbalimbali pamwe na muziki mfano kama ilivyokuwa bima nk,Jumuiya mbalimbali nazo ziamshe burudani nk
17. [09:43, 6/23/2017 Hii itarudisha kirahisi muziki wetu, twahitaji watu wenye uzalendo ktk hili
[09:45, 6/23/2017 Mfano mimi binafsi ningekuwa na uwezo ili kuteka "hadhira " kirahisi, basi ningekusanya wana muziki wote mahiri na ninaojua hawa wapo vzr, ningeingia nao mkataba wa miaka 3-5 ,na wakitoa album, mbili tatu, dah lazima watu wakubali
[09:47, 6/23/2017 Yaan ntafanya km vile "Tanzania all stars " ikishindikana hapo basi tutakuwa tumerogwa.
18. kile kiwanda cha kuunganisha matrekta kibaha kinakuwa na bendi inaitwa Valment jazz band si mchezo
19. [09:51, 6/23/2017 haiwezi kushindikana,ujue kwa hii kauli mbiu ya viwanda inaenda na kukua kwa ajira na kuongezeka kwa mzunguko wa pesa ktk eneo husika hivyo si rahisi kukosa watu,lkn pia lengo la kwanza ni kuburudisha wafanyakazi siku za mapumziko kwa hiyo hata wale wafanyakazi watakaofanya mtoko weekend wanaanzia kwao,na wake zao,watoto ndugu jamaa na marafiki hebu ona hapo
[09:54, 6/23/2017 Ngoja kgt ikue, tumiliki bendi ya mfano
20. Hakika utu uzima dawa
21. Hii nzuri. Monkeys and nami nawaza hizi community centers kwa nini hatuoni umuhimu wake...vijijini pia hali mbaya. Choice ni kushinda kilabu au kanisani haswa msimu usio na shughuli za kilimo
22. Nimependa andiko hili. Sahihi kabisa! Niliwahi kuandika kuhusu uvunjaji wa majengo DSM na kuporomosha sky scrapers, hatukatai lakini tunaondoa historia ya jiji letu ambapo tungeweza kujenga new dsm na kuiacha old DSM kama ilivyo kwani historia ambayo inafundishwa shuleni na picha zilizopo haipo ukija katika uhalisia. Mfano nilifika mji wa Bulawayo Zimbabwe wanao mji unaitwa old pumula na new pumula,ambapo wamefanikiwa kuhifadhi historia ya mji wao hawajaubomoa na Leo ni kivutio tosha cha utalii. Hili nimeliongea Facebook zaidi ya Mara 2. Nashukuru kwa andiko hili kwani linaakisi mawazo yangu kuhusu uhifadhi. Siku njema!
23. [09:05, 6/23/2017 Kabisa! Matokeo yake tunaanza kupambana na changamoto ya foleni,maeneo ya maegesho ya magari,mafuriko katikati ya jiji kwa sababu tu ya kutaka kulazimisha mambo na kuacha uasilia wake! Itaendelea kutugharimu sana
[09:08, 6/23/2017 Kuanzia Zinga,bagamoyo,mlandizi,ruvu,chalinze,kibaha,pugu,kisarawe,chanika na kwingineko pembezoni,pangeweza kujenga new DSM na kuacha jiji kama lilivyokuwa. Leo hii barabara nyingi zimebadilishwa,njia uliyopita mwezi jana ukipita leo unakuta kibao (no entry)! Balaa hili!
[09:13, 6/23/2017 Majengo makubwa yameongezeka tena mengi pale kkoo,lakini miundombinu ipo ileile ingawa kunakipindi wachina waliongeza miundombinu lakini haijasaidia kitu kuna mitaa ukipita Maji ya chooni yanamwagika kana kwamba ni kitu cha kawaida,wazo lakujenga Dar mpya ramani ya kisasa ingekua poa sana
[09:16, 6/23/2017Sugu lifikishe kwa waziri kivuli wa mazingira......

24. Asante Mzee Kitime, umegusa sehemu nzuri na mhimu kwa vijana wa taifa hili hasa ukizingatia vijana wengi wamekuwa na mwamko wa sanaa huku wakijiendesha wenyewe bila msaada wowote toka serikalini, niliwahi kumwambia kitu hiki mwakilishi mmoja toka wizarani alitutembelea hapa nafasi siku Za nyuma, community center Ni mhimu sana kwa vijana hata huku walikoendelea bado vipo na vijana wanatumia hadi leo, viongozi wetu alifanyie kazi siyo vijana wote wapenda soka!!!!!
hizi ni baadhi tu ya mesej zilizotumwa kupitia group za whatasapp. Kuna maoni yanendelea kutolewa kupitia Instagram na hata kupigiwa simu....kuna haja ya kuwaamsha viongozi ili kuwanusuru vijana wa nchi hii kwa balaa zaidi....

Comments