KOFI OLOMIDE KUANZA KUSOTA JELA KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA DANSA WAKE
Posted by
jfk
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
-->
Masaibu
ya Koffi Olomide yamefika pabaya baada ya kuanza kifungo cha miezi 3 akisubiri
uwezekano kifungo kirefu zaidi ambacho upande wa mashtaka unataka kitolewe. Adhabu hiyo ni kutokana nakosa la kumshambulia dansa wake katika uwanja wa
ndege wa Jomo Kenyatta International Airpot(JKIA) siku chache zilizopita.
Hukumu hiyo imetolewa na mahakama moja mjini Kinshasa baada ya malalamiko
kupelekwa mahakamani na Mbunge Zakarie Bababaswe, akisema amefungua malalamika
kwa niaba ya umma wa Kongo. Bababaswe alifanya ‘press conference’ iliyorushwa
kwenye TV akiuliza inakuwaje Kofi yuko huru wakati kuna video inayoonyesha wazi
akimshambulia dansa wake. Inasemekana Mbunge huyo na Kofi zaani walikuwa
marafiki wakubwa lakini waliacha urafiki huo baada ya Kofi na muimbaji wake Cindy
Le Coeur, kudaiwa kuimba nyimbo za kumshushia hadhi Mbunge huyo. Kukamatwa kwa
Kofi kulitokana na amri ya Mwanasheria Mkuu wan chi hiyo. Inasemekana
kumekuweko na kushangiliwa kwa hatua hii nchini kongo na nje ya nchi haswa
katika makundi ya wapigania haki za akina mama. Hakika hatua hii ni pigo kwa
Kofi ukijumlisha kuwa umri wake si mdogo,
Comments