-->
Watayarishaji
wa tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA)
wamezindua uandikishaji wa watakaowania tuzo za AFRIMA kwa mwaka 2016.
Wanaotaka kushiriki katika tuzo hizi wanatakiwa wawe wametuma maombi ifikapo
tarehe 30 July 2016. Hii ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kutolewa na kuna ‘category’
mbalimbali zitakazoshindaniwa. Mwaka huu shughuli za utoaji wa tuzo hizo
utafanyika nchini Gambia, baada ya kufanyika Nigeria kwa mara mbili zilizopita.
Tuzo hizo zimekwisha pata baraka ya Umoja wa Afrika (AU) hasa baada ya Angela
Martins, Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Umoja wa nchi za Kiafrika kutamka wakati
wakati wa uzinduzi wa tuzo hizi kuwa umoja huo utaendelea kukuza mahusiano ya
nchi mbalimbalikwa kutumia tasnia ya ubunifu katika kazi za muziki, na
kwa kuunganisha shughuli hizi katika matamko ya Charter for African Cultural
Renaissance, African Youth Charter na AU Plan of Action on Cultural and
creative industries. Mike Dada, Rais na Executive Producer wa AFRIMA, amewaomba
wasanii, mameneja, maproducer, wenye record labels, na maajent kuwahi
kuwasilisha maombi ya wasanii wao. Alionya kuwa hata msanii akiwa maarufu namna
gani AFRMA haitapokea kazi zilizochelewa kuwasilishwa, na wala AFRIMA
haitawafuata wasanii popote. Tarehe ya kuanza kuwapigia kura wasanii itakuwa tarehe
26 Agosti 2016, na AFRIMA Academy itaanza kupitisha majina tarehe 26 Septemba
2016, na shughuli ya kutafuta washindi itaisha tarehe 5 Novemba 2016.
Kwa
mwaka jana tuzo hizi ziliwawezesha Diamond Platnumz, Charlote Dipanda kupata
tuzo tatu kila mmoja, washindi wengine walikuwa Stanley Enow na Olamide Ukitaka
kushiriki ingia
hapa
Comments