MAISHA NI SIASA ni filamu yenye mlengo wa kisiasa inayoelezea hadithi ya kujitolea, uzalendo, uaminifu na ushujaa, na ina jaribu kutoa changamoto kuhusu nafasi ya mitandao ya kijamii na wanaharakati wake katika siasa za Afrika katika zama hizi za baada ya nchi za Afrika kupata Uhuru, na kuangalia maendeleo ya kujenga demokrasia katika nchi hizi. Filamu hii imetayarishwa na 24Hrs Media, The 7thElement & Kileleni Production, na imeongozwa na Shahid Ansari, washiriki wakiwa Paul Mashauri, Loue Kifanga, Bahati Chando, Violet Mushi, Godwin Gondwe, Carl Bosser, Hudson Kamoga Zenno kahumba na wengine wengi.
Filamu ya MAISHA NI SIASA itazinduliwa katika ukumbi wa Century Cinemax, Mlimani City Jumatano 14 Oktoba 2015 kuanzia saa kumi na nusu alasiri, patakuwepo Red Carpet na vinywaji ambapo wahusika wote katika filamu hii watakuwepo. Inategemewa wageni kama 1000 watahudhuria wakiwemo viongozi na wanachama wa vyama vya siasa, mabloga, wanaharakati, viongozi wa makampuni mbalimbali, wajasilia mali na wapenzi wa filamu.
Ili kuona kionjo cha filamu hii na kujua mengi zaidi kuhusu uzinduzi huu, ingia mtandao wa www.maishanisiasa.co.tz, au ukurasa wa Facebook www.facebook.com/maishanisiasa
Comments