Hatimae mwili wa
Mangair umewasili jana kutoka Afrika ya Kusini ambapo alikumbwa na kifo cha
ghafla akiwa katika hatua za mwisho za kurudi nyumbani baada ya kufanya
maonyesho nchini humo.
Alikuja Dar es Salaam na mwaka 2003 na chini
ya P Funk wa Bongo Records alirekodi kibao kilichomtambulisha rasmi
kilichojulikana kama Gheto Langu na jina la Ngwair likawa rasmi hewani. Ngwair
alitoa album yake ya kwanza 2004 iliyojulikana kama AKA MIMI, album iliyopata
tuzo la Kilimanjaro Music Awards ikiwa ni album bora ya Hiphop , pia album hiyo ilikuwa na wimbo Mikasi
uliyoleta malumbano katika jamii hata kutajwa na BASATA kuwa upigwe marufuku.
Album yake ya pili iliitwa Nge iliyotoka 2009, ikawa na
nyimbo kama CNN na Nipe Dili ambao ulimpatia tuzo lnyingine ya Kilimanjaro
Music Awards ukiwa wimbo bora wa Hiphop.
Leo mwili wake
utaagwa katika viwanja vya Leaders Club na baadae kuelekea Morogoro kwa
mazishi.
MUNGU AMLAZE
PEMA PEPONI AMEN
Comments