Jahazi Modern Taarab

Pamoja na kuwa 'Mfalme ' hakuweko(yuko kwenye ziara ya kikazi Marekani), burudani ya Jahazi ilikuwa palepale katika ukumbi wa Travetine. Muziki ukiporomoshwa katika ile aina mpya ya 'taarab', watu walifurahi. Kitu kimoja kilichokuwa wazi,watu wengi zaidi walikuwa wakicheza nyimbo hizi za 'Taarab' kuliko katika 'dance bands' nyingi. Kitu ambacho ningeshauri wanamuziki wa bendi wafanye utafiti inakuwaje Taarab ambayo asili yake si kucheza, watu wanashiriki kucheza zaidi ya muziki wa dansi ambao nia yake ni watu wacheze.






Comments