TAFF wafanya uchaguzi wa viongozi wao kwa amani

Rais wa Shirikisho Simon Mwakifwamba

Taff- Shirikisho la Filamu Tanzania, mchana huu wamefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi wao, Ifuatayo ni orodha ya viongozi hao.

Simon Mwakifwamba alichaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho hilo. Katika uchaguzi huo pia walichaguliwa wajumbe kumi nao ni

i.                Wilson Makubi

ii.              Mike Sangu

iii.             Christian Kauzeni

iv.             Makame Bajomba

v.              Emmanuel Myamba

vi.             Deosonga Njelekela

vii.           John Kallaghe

viii.          Ally Baucha

ix.             Maureen Mvuoni

x.              Mwanaharusi Hela

Uchaguzi ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa BASATA chini ya usimamizi wa Anjelo Luhala na Omari Mayanga maofisa wa  BASATA. Pamoja na mvua bado uchaguzi ulihudhuriwa na wajumbe wa kutosha na ulifanyika katika hali ya utulibu. 
Kati hali inayoonyesha kuna jitihada zinaendelea za wadau upande wa filamu kuwa katika mikakati ya kujipanga Chama Cha Waandishi wa Filamu Tanzania Tanzania Scriptwriters Association (TASA) nao walifanya uchaguzi tarehe  19/12/2011 VIJANA HALL KINONDONI. Waliochaguliwa ni:-
1. Abdul Maisala -Mwenyekiti
2. Kimela Billa -Makamu Mwenyekiti
3. Samwel Kitang’ala -Katibu
4. Subira O.Nassor Chuu -Mweka Hazina
5. Mike Sangu -Mjumbe
6. Dimo Debwe -Mjumbe
7. Ramadhani King’aru -Mjumbe
8. Badru M Soud -Mjumbe
9. Amos Banzi -Mjumbe
10. Nasir Mohamed -Mjumbe
11. Christian Kauzeni -Mjumbe
12. Pierre Mwinuka -Mjumbe
13. Eric Chrispin -Mjumbe 
Tunawapongeza wote waliochaguliwa kama wajumbe na nafasi nyingine za kiutendaji, tunatarajia kuwa kuchaguliwa kwao kutaleta changamoto za kiutendaji na kusukuma mbele maendeleo ya TASA na TAFF.

Comments