Bongo Star Search yafikia fainali 14 Oktoba





Mkurugenzi wa Benchmark Productions Ritha Paulsen ametangaza rasmi kuwa finali ya BSS Second Chance itakuwa tarehe 14 October 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Katika finali hizo ambazo zitapambwa na msanii kutoka Nigeria N’ABANIA au maarufu kama MR FLAVOUR, wanamuziki wanne waliobakia watashindana na mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shilingi milioni 40, mshindi wa pili milioni 10, na watatu milioni 5.
Watakaoshindana ni Waziri Salum(BSS23), Rogers Lucas(BSS27), Bela Kombo(BSS05) na Hadji Ramadhani(BSS11).
BLOG HII INAWATAKIA KILA LA HERI WASHINDANI WOTE

Comments